Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amesema kuwa wakati umefika sasa wa kutokomeza na kuachana kabisa na masuala yote yanayohusu Ukatili wa Kijinsia na Unyanyasaji kwa ujumla huku akisisitiza kuwa uwepo wao viongozi hapo kwenye Kongamano hilo ni sehemu ya muendelezo wa kupaza sauti na kutambuliwa kuwa binadamu wote ni sawa.
RC Macha ameyasema hayo wakati akitoa salamu za Mkoa katika Kongamano la Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) ambalo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake, Wazee, na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Riziki Pembe Juma ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake na Wanawake Wenye Ulemavu yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Lyakale Hotel iliyopo Manispaa ya Shinyanga.
"Ni wakati sasa umefika kwa sisi sote kuamua kutokomeza kabisa ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kwa ujumla kayika Mkoa wetu huu wa Shinyanga, na kwamba uwepo wetu sote hapa ni sehemu ya muendelezo wa kupaza sauti na kutambuliwa kuwa sisi sote binadamu ni sawa," alisema RC Macha.
Katika hotuba yake Mhe. Riziki alisema kuwa kwa muda mrefu jinsi ya Kike ilikuwa kama imeachwa nyuma sana na hivyo ni wakati sahihi sasa kuongeza nguvu katika kumtambua, kumthamini na kumpa nafasi kwani anaweza na kwamba harakati hizi zilianza miaka 30 iliyopita huko Beijin na sasa tunaona matunda yake na mfano hai tulionao tena wa kuigwa na Mataifa ni kupitia kiongozi wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amedhihirisha kwa vitendo kuwa ni kinara namba moja ndani na nje ya nchi katika nyanja mbalimbali.
Mhe. Riziki ameongeza msisitizo wake kwa wazazi na walezi kuwa, watoto wetu wasaidiwe ili wawezetimiza ndoto zao kwanii Serikali kwa upande wake imeishafanya ikiwemo kujenga mindomhinu ya shule, hosp, vituo vya afya, maji, umeme, uwezeshaji wananchi kiuchumi, kuwatua ndoo na kuni akinamama kichwani imefanya haya yote ili mtoto atimize ndoto yake na kumsaidi pia mama.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa