Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MENEJA wa Jambo Media ndugu Nickson George (kushoto) amefika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha kwa lengo la kujitambulisha na pia kuelezea mikakati ya Jambo Media katika muktadha wa kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha umma ambapo pamoja na hayo pia juu ya programu zinazotarajiwa kutekelezwa hivi karibuni kupitia Jambo Fm 92.7 pamoja na mitandao mingine ya kijamii.
Tarehe 15 Mei, 2024 Jambo Media itazindua rasmi Kampeni ya Jambo FM kuwa Benki, ambapo mgeni rqsmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha hafla ambayo itafanyika katika Ofisi ya Jambo Media iliyopo Kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa