Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka wanawake wote na jamii kwa ujumla kuendelea kupinga, kukemea na kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia katika maeneo wanayoishi au kufanyia shughuli zao, kwakuwa tatizo hili bado lipo miongoni mwa jamii zinazotuzunguuka.
RC MNDEME ameyasema hayo leo tarehe 8 Machi, 2024 wakati akihutubia katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, sherehe iliyofanyika katika viwanja vya Sabasaba Manispaa ya Shinyanga ambapo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vikundi vya wanawake, viomgozi wa Vyama na Dini huku akisisitiza kuwa jitihada za kiondoa ukatili huu zinapaswa kuanza na jamii yenyewe.
"Tunapoadhimisha Siku hii ya Wanawake Duniani, niwatake sotemkwa pamoja kuendelea kupinga, kukemea na kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia ambao bado upo miongoni mwetu na jamii zinazotuzunguuka, kwakuwa juhudi hizi tunapaswa kuanza nazo sisi wenyewe ukizingatia wanaotenda haya matukio tunaishi nao," amesema RC Mndeme..
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita amesema kuwa, wanawake wanaposherehekea siku ya leo, pamoja na mambo mengine lakini pia wanao wajibu wa kumsemea mema na mazuri yote anayoyafanya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwakuwa ameendelea kuwatumikia vema watanzania na kuwaletea maendeleo ya kweli.
Kando ya hayo, RC Mndeme amepokea zawadi na misaada mbalimbali kutoka kwa wadau wakiwemo Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Wakurugenzi wa Halmashauri na Taasisi, Vikundi , shirika lisilo la kiserikali YAWE, Life Water International, Rafiki SDO,TCRS, ADD International na ICS.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa