Wiki ya kutoa elimu na ushauri wa kisheria imezinduliwa katika Mkoa wa Shinyanga mapema leo tarehe 02/02/2019 huku watendaji wa Idara mbalimbali wakitakiwa kutenda haki kwa wananchi ili kupunguza malalamiko kwenye ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amesema wananchi wengi wanakwenda kwenye Ofisi yake na Mkuu wa Wilaya kulalamika kuhusu kutokamilika kwa mashauri yao Mahakamani.
"Nimechoka kusikia Shinyanga ikizungumziwa kwa rushwa rushwa, watu wanakimbia mahakamani kwa sababubhawatendewi haki, wanakuja Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wilaya ndiyo kwenye haki"
Mhe. Telack amesisitiza kuwa, hawezi kukaa akaangalia wananchi wakilalamika watumishi kuwataka rushwa ili kutekeleza majukumu yao..
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa