Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Joyce Ndalichako amesema ameridhishwa na ubora wa majengo pamoja na usimamizi mzuri wa fedha za Serikali kwa kufuatilia kwa karibu kuhakikisha ujenzi wa majengo hayo unalingana na thamani ya fedha.
Akizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa ziara yake jana tarehe 09/11/2019 Mkoani hapa, ambapo amekagua madarasa yaliyojengwa kwa mpango wa lipa kwa matokeo katika shule ya msingi Viwandani na kuweka jiwe la msingi kwenye Ofisi ya Mdhibiti ubora wa shule kwenye Manispaa ya Shinyanga, pamoja na kufungua Ofisi ya mdhibiti ubora katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Mhe. Ndalichako amesema usimamizi mzuri ndiyo kitu cha muhimu katika kusababisha ubora wa majengo.
Serikali ilitoa kiasi cha sh. milioni 152 kwa ujenzi wa kila Ofisi ya mdhibiti ubora lakini katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, imekamilisha Ofisi hiyo ndani ya muda wa miezi miwili na nusu na kutumia kiasi cha sh. 107 na Halmashauri Manispaa ya Shinyanga ambayo ipo kwenye hatua ya ukamilishaji hadi sasa imetumia kiasi cha sh. milioni 91.
"Hiyo inaonesha kwamba, uaminifu na usimamizi mzuri unapata matokeo mazuri kwa gharama nafuu" amesema Mhe. Ndalichako akiupongeza uongozi wa Mkoa na Wilaya kwa kushirikiana kusimamia vema majengo hayo.
Ameongeza pia, dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Watanzania wote wanapata elimu bora ambapo Wadhibiti ubora ndiyo jicho kuhakikisha elimu hiyo inatolewa, lakini kwa muda mrefu walikuwa wamesahaulika hivyo Serikali imetoa shilingi milioni 15. 2 kwa Halmashauri zote nchini kujenga Ofisi za Wadhibiti ubora pamoja na magari 54 yameshanunuliwa ili kuwawezesha kufanya kazi yao kama ilivyo lengo la Serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akimshukuru Waziri Ndalichako kwa Wizara yake kufanya kazi kubwa ya kujenga Ofisi za Wadhibiti ubora amemuomba kuangalia namna ya kuwawezesha wadhibiti ubora kupata fungu la kutosha ili waweze kukagua shule zote hasa za pembezoni,
"Kwa sababu tumesema kipaumbele chetu ni elimu ningependa kuona shule zetu zote zinakaguliwa" amesema Mhe. Telack
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack akisisitiza jambo wakati akimkaribisha Waziri Ndalichako katika Mkoa wa Shinyanga mapema jana tarehe 09/11/2019 Ofisini kwake
Muonekano wa jengo la Ofisi ya Mdhibiti Ubora katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa