Na. Shinyanga RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza D. Tumbo amekutana na timu kutoka Shirika la Msaada wa Watu wa Marekani yaani USAID wakiwa wameambatana na Mkurugenzi pamija na wafanyakazi wengine kutoka Shirika la Pact Tanzania, Shirika la FHI 360, THPS, NACOPHA na SHDEPHA+
Wawakilishi hao wamefika mkoani shinyanga kwa lengo la kutembelea miradi wanayoifadhiri na kuitekeleza katika Halmashauri zilizopp mkoani hapa, ambapo pqmoja na mambo mengine wameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa namna ambavyo imekuwa ikishirikiana katika kuhudumia wananchi wa shinyanga
Kwa upande wake Prof. Tumbo amewashukuru sana kwa ujio wao, kwa namna ambavyo wanatekeleza miradi yao na kwa namna ambavyo wamekuwa wakishirikiana na serikali katika nyakati zote.
Aidha Prof. Tumbo alitumia nafasi hiyo kuwaeleza wageni hao namna ambavyo serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyoleta zaidi ta Trilioni moja mkoa wa shinyanga kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu, afya, miundombinu, uwezeshaji wananchi kiuchumi, nishati, maji nk.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa