KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza D. Tumbo amewataka watumishi mkoani shinyanga kubadilika kifikra, kuongeza ufanisi wa kazi zao pamoja na kuhudumia wananchi vema na lunga nzuri katika ofisi zao.
Prof. Tumbo ameyasema haya alipokuwa akizungumza na watumishi waliopo ofisi ya mkuu wa mkoa wa shinyanga kwa lengo la kupokea, kusikiliza na kutatua changamoto zote wanazokabiliana nazo katika maeneo yao ya kazi pamoja na kukumbushana wajibu na majukumu yankila mmoja.
"Huu ni mwaka mpya wa 2024, ninawaelekeza nyote mbadilike kifikra, ongezeni ufanisi wa kazi, wahudumieni wananchi kwa wema kabisa, tumieni lugha nzuri na mtende haki, kwa kufanya hivi tutakuwa tumetekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi vema kwa wanashinyanga", alisema Prof. Siza Tumbo.
Huu ni muendelezo wa utaratibu wake wa kawaida Prof. Tumbo wa kukutana na watumishi kwa lengo la kupokea, kusikiliza na kutatua changamoto zpte wanazokutana nazo katika maeneo yao ya kazi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa