Na. P. Kasembo, KAHAMA MC.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amemalizia kutoa mkono wa Eid Al - Fitr kwa Makao ya Watoto Yatima katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama na Kishapu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu hii pamoja nao kupitia zawadi hizo ikiwa ni muendelezo ulioanza Machi 30, 2025 ambapo alikabidhi kwa Makao na Makazi yaliyopo Shinyanga Manispaa.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, RC Macha alisema kuwa wao kama wasaidizi wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wameagizwa kupeleka zawadi hizo kwa watoto hao ili kuwashika mkono katika kusherehekea Sikukuu hii na kwamba anatambua uwepo, anathamni, anaheshimu na anawajali sana wao kama sehemu ya jamii na kwamba wao pia kama walivyo watoto wengine wanazo haki na stahiki sawa sawa.
"Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuagiza tuje kuwaletea zawadi hizi ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Sikukuu hii ya Eid Al - Fitr pamoja naye ambapo ametupatia vitu mbalimbali ikiwemo Mchele, Mafuta ya Kupikia, mboga (mbuzi), Sharubati (juice), maji, sabuni na maziwa kwa watoto wachanga hivi vyote ametoa tuwaletee na ametoa salamu zake kwenu kuwa anawapenda sana," alisema RC Macha.
Awali akitoa salamu za utangulizi kwa watoto hao katika nyakati tofauti, Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita aliwaeleza watoto hao kuwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni Kiongozi wa Nchi na Mama wa Watoto wote na ndiyo sababu leo tumekuja na Mhe. RC Macha kuwaletea zawadi hizi maalum kwa siku ya leo na kila mtoto atafurahia naye kwa kuwa kwake watoto wote ni sawa.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi mbalimbali kwa Makao ya Shinyanga Society for Orphanage Centre yaliypo Manispaa ya Shinyanga, Mwadui Home of Vulnerable - Kishapy DC, ZaQahana Orphanage Centre - Kahama MC, Muvuma Children Home - Kahama MC, New Hope Orphanage Centre - Kahama MC, Kahama Peace Orphanage Centre - Kahama MC na Makazi ya Wazee na Wenye Mahitaji Maalum Kolandoto yaliyopo Manispaa ya Shinyanga.
Picha ikimuonesha Mheshimiwa Mboni Mhita, Mkuu wa Wilaya ya Kahama
Sehemu ya muonekano wa watoto wakifurahia zawadi
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa