Na. Paul Kasembo, SHY RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni amefungua Baraza la Wafanyakazi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine lilijadili utekelezaji wa Bajeti ya fedha kwa mwaka 2024 na 2025.
Katika Baraza hilo pia walimualika Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, ambaye katika salamu zake kwa watumishi aliwapongeza kwa kazi wanazozifanya huku akiwasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa umoja, upwndo, ushirikiano na kwamba Serikali inawategemea wao katika kuwahudumia wananchi ambapo watahakikisha wanakuwa na ustawi katika nyanja zote muhimu za kijamii ikiwemo elimu, afya, miundombinu, maji, uwezeshaji wananchi kiuchumi nk.
Kando na hayo, pia watumishi wametakiwa kuwa wabunifu, wazalendo na wenye kuzitumia vema rasilimali za Serikali kwa maslahi mapana ya wananchi na wala siyo vinginevyo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa