Na. Shinyanga RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza D. Tumbo amefungua kikao cha vyama vya ushirika na warajis wasaidizi wa mikoa ya kanda ya ziwa na baadhi ya mikoa ya singida na Tabora kilichofanyika leo 10 Nov, 2023 katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa mkoa lengo ni kuhabarishana juu ya kuanza kwa matumizi ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani huku akiwasisitiza kwenda kuwa wazalendo katika utekelezaji huu ili ulete tija kama serikali ilivyokusudia.
Prof. Tumbo amesema serikali hii ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, yeye mwenyewe Mhe. Rais ameamua kurejesha mfumo huu kwetu ili unufaishe vema pande zote, na kwamba kinachotakiwa kwa viomgozi hawa sasa ni kwenda kuutndea haki katika maeneo yao.
"Niwaagize viongozi wote wa Muungano wa Vyama vya Msingi vya Ushirika kwenda kutanguliza uzalendo, weledi na umakini zaidi katika kutekeleza mfumo huu wa stakabadhi ghalani ili ulete tija kwa pande zote kama ambavyo serikali ilivyo na nia njema na wananchi wake kupitia ninyi," alisema Prof. Tumbo.
Kwa upande wake Mrajis Msaidizi Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace ambaye pia katika kikao hiki alikuwa Mwenyekiti aliwakumbusha washiriki kwenda kuanza maandalizi hivi sasa ya utumiaji wa mfumo huu, huku akiwasisitiza katika kushirikisha makundi yote muhimu katika kuwapatia elimu na taarifa ili wakati utakapofika iwe rahisi katika utekelezaji.
Nao washiriki wa kikao hiki kwa kauli moja wameazimia kwenda kusimamia yale yote waliyokubaliana ili kuleta tija kwao na kwa nyingine za wadau kama ambavyo serikali imekusudia.
Pamoja na RAS Shinyanga, pia kikao kimehudhuriwa na Augustino Mbulumi, Mkurugenzi wa Uendeshaji Soko la Bidhaa Tanzania (TMX), Witness Temba Afisa Udhibiyi Ubora kutoka Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala Tanzania na Robert Nsunza kutoka Masoko na Uwekezaji Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania.
Stakabadhi ghalani ina lengo la kumsaidia mkulima kuuza zao lake kwa bei ya soko, uhakika wa soko, uhakika wa kuhifadhi zao lake na ushindani kulingana na hali ya soko, kujuwa hali ya soko nk.
HABARI PICHA
Prof. Siza D. Tumbo, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga akielezea jambo wakati wa kikao cha viongozi wa vyama vikuu vya ushirika wa mikoa ya kanda ya ziwa na baadhi ya mikoa ya Tabora na Singida.
Bi. Hilda Boniphace, Mrajis Msaidizi Mkoa wa Shinyanga
Sehemu ya viongozi wa vyama vya ushirika wakiwa ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya mkuu wa mkoa wa shinyanga wakati wa kikao
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa