Na. Shinyanga RS.
KATIBU Tawala Mkoa wa Shinyanga, Prof. Siza D. Tumbo, amekutana na viongozi wa TANESCO wakiongozwa na Meneja wa Mkoa, Mhandisi Leo Mwakatobe, pamoja na uongozi wa Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Kahama Shinyanga ( KASHWASA ), ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Mhandisi Patrick Nzamba.
Malengo makuu ya kukutana ni pamoja na kujengeana uwelewa wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya pamoja, kujadili changamoto za taasisi na pia kutafuta utatuzi c wa hangamoto hizo.
Ikumbukwe kuwa, KASHWASA ndio inayotoa huduma ya maji yanayotokea Ziwa Viktoria, na kituo chao cha usambazaji maji kinatumia umeme mwingi wa TANESCO wenye thamani ya zaidi ya Milioni 500 kwa kila mwezi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa