• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RC amuagiza Mwenyekiti wa Kijiji kumtoa mtoto kwenye kazi ya kuchunga ng'ombe

Posted on: January 8th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amemtaka Mwenyekiti wa kijiji cha Ilindi, kata ya Zongomela kuhakikisha mtoto Majebele Masanja anaacha mara moja kazi ya kuchunga ng’ombe na anapelekwa shule.

Mhe. Telack ametoa agizo hilo jana tarehe 07/01/2020 baada ya kumkuta mtoto huyo maeneo ya shule ya Sekondari Ilindi akiwa anachunga ng’ombe badala ya kuwa shuleni ambapo alihojiwa na kusema kuwa anafanya kazi kwa ujira wa sh. 20,000 kwa mwezi na kuwa hasomi kwa sababu mzazi wake hana uwezo.

Akizungumza na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Mji Kahama katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo ambapo ametoa agizo hilo kwa Mwenyekiti huyo, Telack amesema wenyeviti wote wakahakikishe wazazi wanaelekezwa kusimamia mahudhurio ya wanafunzi shuleni.

“Mkazungumze na wananchi, wazazi na walezi kuhusu wanafunzi wasiofika shuleni, mkafanye mikutano ya hadhara na muazimie kusimamia mahudhurio shuleni” amewaambia.

“Haiwezekani wazazi kuacha watoto wanachunga badala ya kusoma, mtoto yule apelekwe shuleni na nitafuatilia” amesema Mhe. Telack.

Aidha, Telack amewasisitiza Wenyeviti wote wa Mitaa na Vijiji kushirikisha wananchi katika shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na kujenga maboma ya madarasa, kusaidia kukomesha matumizi ya madawa ya kulevya na kuwaongoza wananchi bila kuendekeza migogoro isiyokuwa na sababu.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA

    November 13, 2025
  • RC MHITA AKUTANA NA MSANII BANDO MC, APONGEZA JUHUDI ZA KUSAIDIA VIJANA SHINYANGA

    November 11, 2025
  • RC MHITA APONGEZA UONGOZI MPYA WA KANISA LA WASABATO NGBF MKOANI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • WANAFUNZI 29,193 KUFANYA MTIHANI WA UPIMAJI KIDATO CHA PILI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • Angalia zote

Video

RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA

    Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa