Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amefungua maonesho ya nanenane Kanda ya Ziwa Masharikii yanayofanyika viwanja vya Nyakabindi Bariadi mkoani Simiyu huku akiwataka wananchi kutembelea maonesho haya ili wapate elimu, ushauri na maarifa mapya juu ya kuendesha kilimo na ufugaji wa kisasa kwani katika viwanja hivi kuna wataalam wengi mbalimbali kutoka mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Mara na pia Wizara zimeshiriki.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 3 Agosti, 2024 alipokuwa alipokuwa akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Kenan Kihongosi ambaye ndiye mwenyeji wa maonesho haya, alikuwepo pia Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Kanali Evans Mtambi, Makatibu Tawala wa Mikoa yote mitatu, Wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Taasisi na wananchi ambao kimsingi ndiyo walengwa huku akipongeza kwa ujumla namna ambavyo maandalizi yamefanyika kufanikisha maonesho haya.
"Pamoja na pongezi kwa wandaaji wa maonesho haya, lakini niwaombe wananchi wajitokeze kwa wingi hapa kwa siku hizi za maonesho ili wapate elimu, ushauri na utaalam kutoka kwa wabobezi wetu kuhusu namna bora ya kulima, kufuga na kufanya biashara kilimo, na uzuri wake ni kwamba vyote hivi vinafanyika bure bila gharama yoyote,"amesema RC Macha.
Awali akimkaribisha kuhutubia wananchi, RC Kihongosi alisema kuwa uwepo wa maonesho haya Nyakabindi ni fursa kubwa sana kwa wananchi wetu wa Mikoa hii mitatu ya Shinyangq, Mara na Simiyu kwani imekutanisha wataalam wa Serikali, Taasisi na Sekta binafsi
Maonesho haya ya nanenane yanatarajiwa kuhitimishwa ifikapo tarehe 8 Agosti, 2024 ikiwa ni kilele chake kwa nchi nzima huku yakitajwa kuwa na tija zaidi kwa wananchi hususan wakulima ambao watapata fursa ya kukutana na wataalam, taasisi mbalimabali zikiwemo za kifedha na kilimo zenye kutoa elimu, mikopo ya vifaa vya kilimo na namna bora ya kufanya kilimo na ufugaji kuwa wenye tija zaidi kwa rasilimali chache.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa