Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekabidhi Vitendea kazi (Vishikwambi) 262 kwa Maafisa Ugani Kilimo wa Halmashauri sita (6) zinazounda Mkoa wa Shinyanga huku akimshukuru na kumpongeza sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuimarisha na kuwezesha watumishi kutekeleza wajibu kikamilifu.
RC Macha ametoa msisitizo huu tarehe 5 Septemba, 2024 alikuwa akikabidhi vifaa hivyo katika ukumbi wa mikutano uliopo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo pia limehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga CP. Salum Hamduni, vyama vya siasa na wadau wa maendeleo na kuiwasisitiza wataalam hawa kwenda kuvitumia kwa lenho kusudiwa na siyo vinginevyo.
"Tunamshukuru na kumpongeza sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia Vishikwambi ikiwa ni vitendea kazi muhimu kabisa kwa Maafisa Ugani Kilimo, niwaombe sasa wataalam muende kuvitumia kama ilivyokusudiwa na siyo vinginevyo na vikalete tija katika kuwahudumia wananchi wetu," amesema RC Macha.
Vishikwambi hivi vilivyopokelewa na Wakuu wa Wilaya za Shinyanga ni muendelezo wa Serikali katika kuwawezesha watumishi ili waweze kutekeleza kwa ufanisi mkubwa kazi zao katika kuwahudumia wananchi na kuleta tija zaidi ambapo mwaka 2023 Februari Serikali pia iliwapatia maafisa ugani kilimo pikipiki 224 katika Halmashauri zake zote 6.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa