Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ametembea na kukabidhi zawadi ya chakula, vinywaji, sabuni, mafuta na chumvi kwa Kituo cha Kulelea Wazee Wasiojiweza kilichopo Kolandoto Manispaa ya Shinyanga huku akiwahakikishia wazee hawa kuwa Serikali ipo pamoja nao, haina ubaguzi wa aina yoyote na maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya kwamba kila mmoja ataishi kwa furaha na amani zaidi nchini mwao.
RC Macha ameyamesema haya wakati akizungumza na wazee hawa ambao kwa sehemu kubwani kundi maalum wapatao 18 ambapo pamoja na mambo mengine amemtaka Mhandisi wa Manispaa ya Shinyanga kwenda kufanya tathimini ya eneo, kutengeneza mchoro wa jengo la kisasa lenye vyumba 20 ili Serikali iweze kuwajengea wazee hawa ikiwa ni sehemu ya kuboresha makazi yao.
"Nawaagiza wataalam wa Manispaa ya Shinyanga kufika hapa Kituo cha Kulelea Wazee - Kolandoto ili kufanya tathimini na kuchora ramani ya jengo la vyumba 20 ili Serikali iweze kuwajengea nakuboresha makazi yao," amesema RC Macha.
Kituo cha Wazee Kolandoto kilianzishwa rasmi mwaka 1977 ambapo kimekuwa kikihudumiwa na Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum na kwa sasa walengwa wote waliopo hapa wanapata chakula kuazia asubuhi, mchana na usiku.
Pia wamepatiwa Bima ya afya ambapo wanapata huduma ya matibabu bure wakati wote na kwa msisitizo wa RC Macha kuanzia sasa Serikali ya Mkoa wa Shinyanga itakitazama kwa ukaribu zaidi Kituo hiki.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa