Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha, leo tarehe 23 Julai, 2024 amekutana na Kamati ya Maandalizi ya Shycom Alumni Marathon iliyofika Ofisi kwake kwa lengo la kujitambulisha, kutambulisha tukio la Shycom Alumni Marathon ambapo pamoja na kuwapongeza kwa kuja wazo hili lakini pia Rc Macha amewaahidi ushirikiano wakati wote ili kufanikisha zoezi hilo.
Shycom Alumni Marathon ni mbio zenye lengo la kuhamasisha jamii, kuleta mshikamano miongoni mwa wanachuo waliowahi kusoma Shycom na kufanya changizo katika kuboresha miundombinu na afya ya chuo.
Shycom Alumni Marathon itafanyika tarehe 21 Septemba 2024 katika viwanja vya CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
HABARI PICHA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha
Picha ikiwaonesha wajumbe wa kamati ya maandalizi
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa