Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amekutana na viongozi wa Chama cha Viziwi Tanzania waliofika kwa lengo la kujitambulisha kwake pamoja na kuelezea dhumuni la uwepo wa maadhimisho ya Wiki ya Viziwi Duniani ambayo Kitaifa yanafanyika hapa mkoani Shinyanga kuanzia tarehe 23 - 28 Septemba, 2024.
Akitoa taarifa fupi ya maadhimisho haya, Mwenyekiti wa CHAVITA Bi. Celina Mlamba ameanza kwa kumshukuru na kumpongeza Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali CHAVITA ambapo wanaendelea kupata nafasi mbalimbali katika utumishi wa umma, elimu afya nk. huku wakishukuru pia RC Macha kwa namna ambavyo anashirikiana na CHAVITA Shinyanga na Taifa na kwamba kufanyika kwa tukio hili hapa Shinyanga ni kilelezo kuwa wanatambua na kuthamini msaada mkubwa wanaoupata kwa Serikali ya Mkoa na Taifa pia na kwamba sasa unaiweka Shinyanga kwenye ramani ya Mikoa inayoijali na kuiunga mkona zaidi CHAVITA.
Haya yametokea leo tarehe 24 Septemba, 2024 ikiwa ni siku moja kuelekea ufunguzi rasmi wa Wiki ya Viziwi Duniani katika hafla itakayofanyika kwenye ukumbi wa mikutano uliopo jengo la CCM Mkoa wa Shinyanga ambapo wito umeendelea kutolewa kwa wadau kushiriki kikamilifu.
Kwa upande wake Mwakilishi UNDP Tanzania Bi.Ghati Horombe amesema kuwa UNDP itaendelea kushirikiana na asasi za watu wenye ulemavu kwani wanthamini na wataendelea kushirikiana ili kuhakikisha malengo ya kundi hili yanafikiwa vema ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya uchumi wa kidijitali kwa vijana 150 kutoka katika kundi hili.
Akihitimisha mazungumzo haya RC Macha amewakaribisha sana mkoani Shinyanga wageni wote na kwamba Serikali inatambua na kuthamini sana mchango wa kundi hili na kwamba wataendelea kushirikiana nao wakati wote, na kwamba maadhimisho haya yatafana zaidi kwakuwa maandalizi yote yamekamilika tayari. Kauli mbiu ya mwaka 2024 inasema "Ungana Kutetea Haki za Lugha ya Alama"
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa