Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amemkaribisha mkoani Shinyanga Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa (MB) na kumueleza kuwa, anamshukuru na kumpongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutengeneza na kuboresha miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Shinyanga.
RC Macha pia amemjulisha juu muendelezo wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara ikiwemo ile ya Kahama hadi Kakola pamoja na ile ya Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ambayo inaunganisha na Mkoa wa abora huku akisisitiza kuwa, kukamilika kwake kunachechemua uchumi wa wananchi wa Mikoa hii jirani ikiwemo Tabora na Geita.
Kwa upande wake Mhe. Bashungwa amesema kuwa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kutengeneza na kuboresha miundombinu ya barabara kaa Watanzania wote wakiwemo wa Mkoa wa Shinyanga lengo ni kuhakikisha wananchi wanakuwa na maisha bora zaidi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa