Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha mapema leo Februari 15, 2025 amemkaribisha mkoani Shinyanga Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambaye aliwasili mkoani hapa akielekea mkoani Simiyu kwa ziara ya siku moja.
Mhe. Majaliwa, pamoja na mambo mengine ameahidi kurejea Shinyanga Februari 16, 2025 ili aweze kutembelea na kuona mwenendo wa ujenzi wa jengo la abiria uwanja wa ndege pamoja na na ukarabati mkubwa wa Uwanja wa ndege uliopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa