Na. Paul Kasembo - KISHAPU.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amepokea mchango wa Darasa 1 na Madawati 20 kutoka CRDB BANK - Shinyanga ikiwa ni sehemu ya mrejesho utokanao na faida baada ya makato ya TRA yaani CSR iliyogharimi Tzs. Mil. 20 ambapo pamoja na kuwashukuru, kuwapongeza na kuwaomba tena CRDB lakini pia aliwataka wananchi kuvitunza ili viwanufaishe na wengine.
RC MACHA ameyasema haya tarehe 9 Aprili, 2024 alialikwa katika hafla ya kukabidhiwa mchango huu katika Kijiji cha Kiloleli Kata ya Kiloleli katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo pamoja na mambo mengine RC Macha ameahidi kupeleka tofali elfu 4 kwa ajili ya umaliziaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 2 na ofisi moja ujenzi ambao umefikia hatua ya msingi.
"Tunawashukuru sana CRDB BANK Tawi la Shinyanga kwa mchango wenu wa darasa 1 na madawati 20, mchango ambao umehamasishwa na Ndg. Madaha Chaba ambaye ni mzaliwa wa kijiji hiki na mtumishi wa CRDB BANK Makao Makuu, hakika mmeacha alama kwa jamii yetu, nasi Serikali tutaendelea kushirikiana nanyi wakati wote," RC MACHA.
Kwa upande wake Meneja wa CRDB BANK Kanda ya Magharibi Mchumi Jumanne Wagana amesema kuwa Benki yao Tawi la Shinyanga iliamua kutekeleza hili baada ya kupokea wazo kutoka kwa mtumishi mwenzao na huu ni utaratibu wa kawaida kabisa wa Benki yao kurejesha sehemu ya faida kwa jamii ili kuweka miradi yenye kunufaisha wananchi katika eneo husika huku akiwasisitiza wananchi kutunza rasilimali hizi.
Shule ya Msingi Kiloleli kilianzishwa rasmi mwaka 1956 ina jumla ya wanafunzi 1949, walimu 9 na ilianza rasmi ujenzi wa darasa hili Mei, 2023 lenye madawati 20. Kukamilika kwa darasa hili kunatajwa kupunguza msongamano kwa wanafunzi katika shule hii.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa