Na. Paul Kasembo, SHINYANGA MC.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Anamringi Macha amepokea Nyaraka nyingjne 118 kutoka kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi zilizobeba kero za wananchi wa Wilaya ya Shinyanga na kuahidi kuwa atakaa na wataalam kuhakikisha zinafanyiwa kazi moja baada ya nyingine.
RC Macha ameyasema haya leo tarehe 11 Oktoba, 2024 baada Balozi Dkt. Nchimbi kupokea kero kutoka kwa wananchi akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi ya Town Manispaa ya Shinyanga ambao ulilenga kupokea, kusikiliza na kutatua kero zao ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.
“Nimepokea Nyaraka hizi zilizobeba kero za wananchi wa Wilaya ya Shinyanga na mimi nakuahidi Katibu Mkuu kuwa, nitashirikiana na wataalamu wangu ili kuanza kuzifanyia kazi moja baada ya nyingine ili kuhakikisha kero zao zote zinatatuliwa kufikia mwisho wa mwezi huu Oktoba wananchi hawa wataanza kupigiwa simu za kuwataarifu kuwa kero zao zimepatiwa ufumbuzi,” amesema RC Macha.
Balozi Dkt. Nchimbi amehitimisha ziara yake ya siku 3 hapa mkoani Shinyanga, ambapo alianza na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, Kahama Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ambapo atapokea, kusikiliza na kutatua kero zao katika eneo la Maganzo.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa