Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha amekabidhiwa samani za ofisi 397 na Shirika la Tanzania Health Promotion and Support (THPS) kupitia mradi wa Afya hatua unaofadhiliwa na mpango wa dharura wa Rais wa Marekani wa kupambana na Maambukizi ya virusi vya Ukimwi na Kifua Kikuu (PEPFAR), Kupitia kituo cha kudhibiti Magongwa (CDC) Tanzania huku akiwapongeza na kuwashukuru kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika Sekta mbalimbali ikiwemo Afya.
Macha amepokea samani hizi tarehe 19 June, 2024 hafla iliyofanyika katika Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga huku akizitaja samani hizi kuwa ni Kabati za kutunzia Mafail, viti, Meza, Benchi za kukaa wagonjwa wakisubiri huduma, kabati ya kuhifadhia dawa zote zikiwa na thamani ya shilingi 295,326,860.
"Nwashukuru sana THPS kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika Sekta mbalimbali ikiwemo Afya jambo ambalo litaboresha utoaji wa huduma kwa wananchi wetu wa Shinyanga na maeneo jirani,"amesema RC Macha.
"RC Macha amesema vifaa hivi vinatakiwa kutunzwa hata mgonjwa akija akaa sehemu nzuri kusubiri matibabu itakuwa vizuri na nakuona ahueni kwake nawaomba kusiwepo eneo la kurundika vifaa hivi kuwa chakavu vitunzwe na watumishi wasife moyo kutekeleza majukumu yao hata kama wachache," RC Macha amesisitiza.
Kwa upande wake Meneja mradi afya hatua kutoka THPS Mkoa wa Shinyanga Dr. Amos Scott akisoma hotuba mbele ya mgeni rasmi na kukabidhi Samani za hospitali amesema hadi kufikia mwezi Machi 2024 wamefikiwa wataalamu ambao wapo kwenye vitengo vya Famasia, Maabara na takwimu ya jumla yao ni 92 na kuwafikia wapokea huduma za tiba na matunzo 70,089.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa