Na. Paul Kasembo, IGUNDA - USHETU
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha amewasili katika Kijiji cha Igunda, kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu ambapo ataongoza Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya Wazee Duniani ambapo kwa Mkoa wa Shinyanga yanafanyika hapa Igunda.
RC Macha akiwa katika maadhimisho haya atapata wasaa wa kupokea maandamano ya wazee, kukagua mabanda mbalimbali, kupokea taarifa fupi ya siku ya leo kutoka kwa Dr. Yudas Ndungile ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa, taarifa ya wazee yao na baadae atazungumza na wazee wote wa Mkoa wa Shinyanga kupitia hadhara hii.
Kauli mbiu ya mwaka huu ya maadhimisho haya inasema “Tuimarishe Huduma kwa Wazee: Wazeeke kwa Heshima”. Nasi sote tunatambua umuhimu wa vijana, familia, jamii, wadau na Serikali kwa ujumla kutoa huduma bora za kiafya, kiulinzi, kijamii, kisaikolojia, kiroho ili wazee waweze kuzeeka kwa heshima.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa