Na. Paul Kasembo, SHY RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha leo tarehe 15 Mei, 2024 amezindua rasmi msimu wa Gangamala wenye miamala ya maudhui katika Studio ya Jambo FM Redio iliyopo Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga
Msimu wa Gangamala umebuniwa kwa lengo kuwafanya Wanashinyanga kujituma, kuchapa kazi ili wawe na maisha fresh/bora zaidi.
RC Macha pia ameongeza sana mmiliki wa Jambo Group kwa kazi nzuri anayoifanya ya uwekezaji mkubwa katika Mkoa wa Shinyanga jambo ambalo amesema limeweza kuzalisha ajira nyingi kwa vijana na wakazi wa Mkoa wa Shinyanga na Mikoa mingine sanjari na kuongeza pato la Serikali katika kulipa kodi.
Jambo FM Redio inatajwa kuwa na wasikilizaji 80% ya vijana na 20% ya makundi mbalimbali imekuwa ni kilelezo bora kahisa kwa tasnia ya habari nchini na nje ya nchi kwakuwa na ubora wa studio zake na ubunifu wa vipindi kwa ujumla.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa