• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RC. MBONI ATOA WITO KWA TISEZA KUTANGAZA FURSA KUU YA KONGANI YA UWEKEZAJI BUZWAGI

Posted on: July 5th, 2025

Sabasaba 2025.

Katika mwendelezo wa ziara katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita ametoa wito mahsusi kwa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kuweka msisitizo katika kutangaza mradi mkubwa wa Kongani ya Uwekezaji Buzwagi, ambao unatarajiwa kuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kiuchumi kwa Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la TISEZA katika viwanja vya Sabasaba, RC. Mboni alieleza kuwa Kongani ya Buzwagi ni fursa adimu ya uwekezaji inayojengwa kwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali ya Mkoa na Kampuni ya Barrick Tanzania, ambayo hapo awali iliendesha mgodi wa dhahabu katika eneo hilo.

“Pamoja na kuwapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya TISEZA katika kutangaza maeneo maalum ya kiuchumi, natumia fursa hii kutoa rai kwenu kuiangazia kwa uzito stahiki Kongani ya Uwekezaji Buzwagi. Mkoa wa Shinyanga una mpango kabambe wa utekelezaji wa mradi huu kwa kushirikiana na Barrick Tanzania, tukilenga kutimiza kwa vitendo dira na maono ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Tanzania yenye uchumi wa viwanda na fursa kwa wote,” alisema Mhe. Mboni.

Aidha, Mhe. Mboni alibainisha kuwa Shinyanga ipo tayari kupokea wawekezaji kwa sasa kutokana na mazingira wezeshi yaliyowekwa na Serikali ya Awamu ya Sita. Alieleza kuwa Mkoa una rasilimali zote muhimu kwa uwekezaji ikiwemo:

Ardhi kubwa na salama kwa uwekezaji, upatikanaji wa maji na nishati ya umeme wa uhakika, miundombinu ya kisasa ikiwa ni pamoja na barabara, uwanja wa ndege wa Shinyanga na Kahama, na mtandao wa mawasiliano ya uhakika, nguvu kazi ya kutosha na yenye ari.

 “Dhamira yangu kama Mkuu wa Mkoa, na dhamira ya Mkoa kwa ujumla, ni kuhakikisha tunawahamasisha na kuwakaribisha wawekezaji kuja Shinyanga na katika Kongani ya Buzwagi ambayo ni mfano wa dira mpya ya kiuchumi, ambapo mazingira rafiki ya uwekezaji yanapatikana kwa urahisi na usalama,” aliongeza RC, Mboni.


Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM APONGEZA USHIRIKI WA MKOA WA SHINYANGA KATIKA MAONESHO YA SABASABA.

    July 06, 2025
  • RC. MBONI ATOA WITO KWA TISEZA KUTANGAZA FURSA KUU YA KONGANI YA UWEKEZAJI BUZWAGI

    July 05, 2025
  • MHE. RIDHIWANI KIKWETE AWAKARIBISHA WANANCHI KUTEMBELEA BANDA LA MKOA WA SHINYANGA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

    July 05, 2025
  • KATIBU TAWALA WILAYA YA KAHAMA AWAPONGEZA WASHIRIKI WA MAONESHO YA SABASABA 2025 KUTOKA MKOA WA SHINYANGA

    July 05, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa