• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RC MHITA AKABIDHI MAGARI 5 MAPYA KWA JESHI LA ZIMAMOTO SHINYANGA, ASEMA YATASAIDIA KUOKOA MAISHA ZAIDI

Posted on: October 20th, 2025

Na Johnson James, Shinyanga

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita @mboni_mhita kwa niaba ya wananchi wa mkoa huo, amezindua na kukabidhi rasmi magari matano mapya kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuboresha huduma za dharura na uokoaji mkoani humo.

Zoezi hilo limefanyika leo Octoba 20,2025 katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambapo RC Mhita aliwataka maafisa wa Zimamoto kuyatunza magari hayo na kuyatumia kwa ufanisi mkubwa, huku akiwaasa wananchi kuyatumia kwa wakati sahihi pale kunapotokea majanga kama moto au ajali.

"Magari haya ni kwa ajili ya kuokoa maisha. Tunahitaji ushirikiano kati ya jamii na Jeshi la Zimamoto. Wananchi watumie huduma hizi kwa wakati, na Jeshi lihakikishe magari haya yanatunzwa vizuri kwa manufaa ya wote," alisema Mhita.

Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga, Thomas Majuto, amesema ujio wa magari hayo ni ukombozi mkubwa kwao kwani awali walikuwa na magari mawili pekee, lakini sasa wamefikia matano, hali itakayoongeza ufanisi kwenye shughuli za uokoaji.

Magari yaliyokabidhiwa ni pamoja na:

- Gari kubwa la kuzimia moto

Magari mawili ya kubebea wagonjwa

- Gari dogo la mitambo ya mawasiliano

- Gari la ukaguzi

Majuto amesema ujio wa magari hayo pia unapanua uwezo wa kufika maeneo mengi kwa haraka na kutoa huduma za kisasa, na hivyo kusaidia kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa majanga.

RC Mhita amesisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan itaendelea kuboresha huduma za uokoaji nchini, ili kuhakikisha maisha na mali za wananchi zinalindwa ipasavyo.

Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA

    November 13, 2025
  • RC MHITA AKUTANA NA MSANII BANDO MC, APONGEZA JUHUDI ZA KUSAIDIA VIJANA SHINYANGA

    November 11, 2025
  • RC MHITA APONGEZA UONGOZI MPYA WA KANISA LA WASABATO NGBF MKOANI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • WANAFUNZI 29,193 KUFANYA MTIHANI WA UPIMAJI KIDATO CHA PILI SHINYANGA.

    November 07, 2025
  • Angalia zote

Video

RC MHITA AWAHAMASISHA WAFANYABIASHARA NA WAWEKEZAJI KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIUCHUMI MKOANI SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA

    Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa