Tukio hilo lilifanyika mara baada ya hafla fupi ya mapokezi ya vikombe hivyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo Mhe. Mhita amewapongeza wanamichezo hao kwa kuonyesha uzalendo, mshikamano na nidhamu katika kuiwakilisha vyema Shinyanga.
“Nimefarijika sana kuona Shinyanga inarejea na vikombe. Hii ni ishara kuwa tunakwenda mbele na tukijipanga vizuri zaidi, naamini tutakuwa mabingwa wa jumla katika miaka ijayo. Ofisi yangu itaendelea kuwa bega kwa bega nanyi,” amesema Mh. Mhita.
Timu ya RS Shinyanga Sport Club imeshinda kikombe cha ubingwa wa kitaifa kwa upande wa mchezo wa karata (wanaume) na kikombe cha mshindi wa tatu kwa upande wa wanawake katika mchezo huo huo.
OFISI YA MKUU WA MKOA, MKOA WA SHINYANGA, 04 MTAA WA BOMA
Anuani: P.O.Box 320, 37180,SHINYANGA, TANZANIA
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa