Na. Shinyanga RC
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme leo tarehe 20 ametembelea, kukagua na kuagiza kukamilishwa haraka kwa ujenzi wa Sekondari mpya ya Nyahanga iliyopo Kahama Manispaa ambayo itagharimu zaidi Mil. 603 jamno ambalo litakwenda kuwaondolea usumbufu wanagunzi waliokuwa wakifuata elimu mbali zaidi.
Pamoja na pongezi kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mhoni Mhita @mboni_mhita kwa kazi nzuri anayoifanya ya usimamizi na ufuatiliaji wa miradi, lakijni pia amemuagiza ahakikishe kuwa maelekezo aliyoyayoa yanatekelezwa huku akiwataka kujenga Tangi la maji kwa ajili ya kuhifadhia maji wakati wakisubiria Mamlaka ya MajiSafi na Usafi wa Mazingira Kahama - KUWASA kuwasogezea huduma ya maji shuleni hapo jambo ambalo litapunguza adha inayotokea hivi sasa ya upatikanaji wa maji.
"Nakuagiza Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni kuhakikisha ujenzi wa shjle hii mpya ya Nyahanga inakamilika haraka kwa ubora, viwango kwa kuzingatia muda mliokubaliana na kwa bajeti ileile," alisema Mhe. Mndeme.
Kando na agizo hiko, lakini pia Mhe. Mndeme amewataka mafundi wanaofanya kazi ya ujenzi shuleni hapo kutanguliza uzalendo wakati wa utendaji kazi wao ili thamani ya majengo hayo ionekane kwa wananchi, wazingatie muda na bajeti waliyokubaliana kwakuwa wao pia ni sehemu ya jamii.
Hii ni ziara ya mwisho kwa Wikaya ya Kahama akiwa ameongoza na mwenyeji wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita, Kamati ya za Usalama, uongozi wa CCM Kahama wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Halmashauri pamoja na wakuu wa Taasisi mbalimbali ikiwamo Tarura, Tanesco, Kuwasa, Vyama vya Ushirika nk.
Ziara ambayo imemuisha Halmashauri 3 ikiwemo Kahama Manispaa, Ushetu na Msalala ambapo pamoja na mambo mengine lakini pia alikagua miradi mbalimbali ya elimu na afya na miundombinu, kuiwekea mawe ya msingi, kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa maeneo hayo.
PICHA NA MATUKIO YAKIONESHA MHE. MNDEME AKIWA SHULE MPYA YA NYAHANGA - KAHAMA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa