MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka wananchi mkoani Shinyanga kuitunza miundombinu ya barabara ikiweo na kuzitunza alama za barabarani kwa maendeleo endelevu sanjali na kuwataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kandokando ya hifadhi ya barabara.
Mhe. Mndeme amesema jukumu la kutunza miundombinu ya barabara ni la kila mtu, sababu barabara ni kichocheo kikubwa cha maendeleo endelevu na ukuaji wa uchumi, na kuwataka wananchi waache kufanya uharibifu wa barabara p Barabara,kupitisha Mifugo na Kung’oa alama za usalama.
“Nawaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga muitunze miundombinu ya barabara, muache kufanya shughuli za kibinadamu kando ya barabara, biashara, kupitisha mifugo hasa kwenye lami, magari mazito na kutupa taka kwenye mitaro ya maj, nanyi Tanroad na Tarura muwe mnazibua mitaro pamoja na madaraja kabla mvua ili maji yaweze kutembea kwa kasi”, amesema Mhe. Mndeme.
Kwa upande wake Meneja Wakala wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA) Mkoa wa Shinyanga Eng. Oscar Mlekwa amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024 kimetengwa kiasi cha fedha zaidi ya Tzs. Bilioni 16.7 kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ya barabara mkoa wa shinyanga.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akielezea jambo wakati wa kikao
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa