Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme ameipongeza Jambo FM inayorusha matangazo yake kutoka katika Manispaa ya Shinyanga kwa kazi kubwa na nzuri ya kuhabarisha, kuelimisha na kurudisha umma kupitia masafa ya 92.7 MHz.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa Kituo hicho cha Redio tukio ambalo lilitanguliwa na mazoezi ya Joggin kutoka SHY COM mpaka VETA na kurudi hadi eneo la Mataa ambapo alishriki zoezi la kupanda miti eneo hilo ikiwa ni ishara ya ufunguzi wa kituo sambamba na kutunza mazingira katika Mkoa wa Shinyanga huku akiwaahidi kuwapatia ushirikaino wakati wote.
"Nawapongeza sana Jambo FM na Jambo Food Product kwa ujumla kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa wananchi wa Mkoa huu wa Shinyanga na Tanzania kwa ujumla wake ya kuhabarisha umma, kuelimisha na kuburudisha huku Jambo Food Product mkizalisha ajira kwa wananchi pamoja na kukuza uchumi kwa wananchi na kuongeza pato la Taifa, hongereni sana Jambo," alisema Mhe. Mndeme.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi alisema kuwa, Jambo FM wamekuwa wadau muhimu sana wakati wote katika utekelezaji wa kazi za habari kwa maeneo haya huku akiwataka kuendelea na utamaduni huu kwa maslahi mapana kwa wananchi.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa