Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Cnristina Mndeme amekabidhi Majiko ya gesi 600 yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye ulemavu) kutoka Kata zote 17 za Shinyanga Mjini huku akimpongeza sana kwa msaada huo na kuwajali wajasiliamali hao.
Hafla hii fupi imefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo jengo la makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga na kudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama, Serikali na Dini.
Mhe. Mndeme amesema kwamba kitendo cha Mhe. Katambi kujitoa na kuwaletea majiko ya gesi wajaliamali hao ni cha kuigwa chenye lengo la kuboresha kazi zao, kutunza mazingira kwa kuachana na matumizi ya nishati ya kuni au mkaa na kuanza kutumia nishati ya gesi ambayo inatajwa kwenda kurahisisha maisha ya wana Shinyanga Mjini.
"Ndugu zangu wana Shinyanga, kwa pamoja tuna kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza sana Mhe. Katambi kwa msaada huu aliotuletea wajasiliamali wa Jimbo la Shinyanga kwa kweli twendeni tukabadilishe mfumo wa matumizi ya nishati ya kuni na mkaa na sasa tuendelee na nishati ya gesi ili tuweze kutunza mazingira na maisha yetu yabadilike na kuwa ya kisasa," alisema Mhe. Mndeme.
Kwa upande wake Mhe. Katambi alisema kwamba, anawiwa kutoa majiko ya gesi hayo yenye thamani zaidi ya Milioni 500 kwa wajasiliamali hao kutoka kata zote za jimbo ili kuweza kuleta chachu ya uchumi, kutunza mazingira na kuachana na nishati ya kuni au mkaa ambayo yaweza kuleta madhara.
Kukabidhiwa huku kwa mitungi ya gesi 600 kwa wajasiliamali hawa inakwenda kuimarisha na kuboresha kazi zao katika kada mbalimbali ikiwamo mama lishe, baba lishe, wauza kahawa pamoja na makundi maalumu na wanachi mbalimbali waliobahatika katika Jimbo la Shinyanga
Mhe. Patrobas Katambi akielezea jambo wakati wa hagla ya uyoaji majiko ya gesi 600 kwa wajasiliamali
Picha ikionesha sehemu ya mitungi ya gesi 600
Mmoja wa wanufaika wa majiko ya gesi yaliyotolewa na Mhe. Katambi
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa