Na. Shinyanga RS
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ametembelea na kukagua ukarabati wa Bwawa la Mwalukwa lililopo Kata ya Mwalukwa Halmashauri ya Shinyanga na kuagiza ukamilishwaji haraka wa bwawa hili ifikapo Oktoba 15, 2023 ili lianze kunufaisha jamii inayoizunguka pamoja na mifugo huku akionya wananchi kuacha kabisa kufanya shughuli za kibinadamu kandokando mwa bwawa na badala yake watunze vyanzo vya maji eneo hili.
Mhe. Mndeme ameyasema haya wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Kata ya Mwalukwa, msimamizi wa mradi huu, mafundi wanaojenga bwawa pamoja na wananchi waliokuwa eneo la mradi huu, ambapo pamoja na kupokea taarifa ya ukarabati wa bwawa lakini alimtaka msimamizi wa mradi huu Ndg. Islael Chafumbwe kutoka Wizara ya Maji kuharakisha ukamilishaji wa mradi huu ili kufikia Oktoba 15, 2023 ukarabati uwe umekamilika kama ulivyokusudiwa.
"Niwapongeze wana Kata ya Mwalukwa kwa kupata mradi huu mzuri na wenye tija kwenu ambao unagharimu zaidi ya Milioni 69 fedha kutoka Serikali inayotekelezwa kupitia Wizara ya Maji na Bonde la Maji Bonde la Kati na ambao utanufaisha wakazi zaidi ya elfu 22 na mifugo zaidi yq elfu 13. Lakini nawaagiza kukamilisha mradi huu haraka ili kufikia Oktoba 15, 2023 ukarabati uqe umekamilika tayari kwa matumizi," alisema Mhe. Mndeme.
Bwawa la Mwalukwa linatekelezwa ili kuwezesha upatikanaji wa maji ya uhakika wa wastani wa mifugo nje ya hifadhi ya bwawa kwa kujengewa Mabirika yatakayowezesha mifugo kupata maji ya uhakika wakati wote na kwa matumizi ya nyumbani pia ambapo linatarajiwa kutoa huduma kwa mifugo zaidi ya elfu 13 na watu zaidi ya elfu 22.
Kukamilika kwa bwawa hili kutaongeza ujazo wa lita hadi kufikia 293,651,980 kutoka ujazo wa lita 71,573,020 za awali wakati lilipokuwa na urefu wa mita 2.25 kwa maelezo hayo kunaonesha kutakuwa na ongezeko la ujazo mara nne ya ujazo wa awali hivyo kuimarisha zaidi utoaji huduma kwa wana jamii na mifugo yao.
Hili ni bwawa linalotekelezwa kupitia wataalam wa ndani kwa kuboresha kwa Kingio la maji (TUTA) lenye kimo cha mita 3.50 na urefu wa mita 410, kuboresha tuta linalozuia utoro wa maji wenye upana wa mita 42 ili kuwezesha kuhifadhi maji.
HABARI NA MATUKIO
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa