RC MNDEME AKUTANA NA WANAWAKE WA KIISLAM MKOA WA SHINYANGA
Na. Shinyanga RS.MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amekutana na Wanawake wa Jumuiya ya Kiislam Shinyanga na kuzungumza nao mambo mbalimbali ikiwemo namna ambavyo serikali ya awamu sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania livyoleta fedha zaidi ya Trilioni 1 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika mkoa wa shinyanga.
Mhe. Mndeme amewaeleza kuwa serikali inawajali sana wananchi wa shinyanga ambapo imeboresha zaidi huduma katika sekta ya afya, elimu, maji, miundombinu ya barabara na uwezeshaji wananchi kiuchumi nk.
Aidha Mhe. Mndeme amewataka kuishi vizuri, kuwajali na kuwafunda watoto wetu wadogo na vijana ili kuzuia mmomonyoko wa maadili, kuepuka na kuacha tabia zisizofaa, zisizofuata maadili na utamaduni wa kitanzania, kukemea na kuzuia kabisa ukatili wa aina yoyote katika maeneo wanayoishi.
Aidha amewaomba kuendelea kumuombea heri na afya njema wakati wote na waendelee kumuunga mkono katika utekelezaji wa majukumu yake ya kuwahudumia wananchi wa shinyanga na tanzania kwa ujumla.
"Ndg zangu akina mama, hakika Rais wetu Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan ameifanyia mema mengi na anaendelea kuijali sana shinyanga na hata sasa ninapoongea hapa tumepokea zaidi ya Trioni moja kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa mkoa wetu. Hakika ni kumshukuru sana na tuendelee kumuombea wakati wote ili aifanye kazi ya watanzania bila kuchoka," alisema Mhe. Mndeme.
Akitoa salamu za jumuiya hii Bi. Aisha Juma amesema kuwa, kipekee kabisa na kwa umoja wao wanamuunga mkono na kumuombea kila siku Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee, kuwahudumia na kuwaletea maendeleo wananchi wa tanzania, kwakuwa kazi zake wanaziona, wanazikubali na hivyo wanamshukuru sana.
"Tunaendelea kumuunga mkono na kumuombea wakati wote Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili aendelee kuwahudumia na kutuletea maendeleo sisi wananchi wa shinyanga na Tanzania kwa ujumla," alisema Bi. Aisha Juma.
Kando na hayo pia Mhe. Mndeme ameahidi kuchangia mifuko 100 ya saruji kwa ajili ujenzi wa ukumbi wa jumuiya hiyo wilayani Kahama.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa