Na. Shinyanga RS
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amemuagiza Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi. Hilda Boniphace kuvifufua vyama vya ushirika 12 vilivyolala kwa kutolipa madeni Benki na aviimarishe badala ya kuanzisha vyama vingine.
Mhe. Mndeme ameyasema haya leo wakati alipokuwa akizungumza na uongozi, watumishi, viongozi wa vyama vya ushirika na baadhi ya wakulima wakati alipofanya ziara katika Chama cha Ushirika Kahama - KACU.
"Nakuagiza Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga uvifufue vyama hivi 12 vinavyotajwa kwenye taatifa hii, uviimarishe na kisha uvisimamie kikamilifu viwe na nguvu kama awali na kufanya kazi vvema badala ya kuanzisha vyama vingine vipya," alisema Mhe. Mndeme
Awali kisoma taatifa mbele yake Meneja wq Chama Kikuu cha Ushirika Kahama Ndg. Abdul Ally alimjulisha Mgeni rasmi juu ya uwepo wa Vyama vya Msingi 12 vilishindwa kurejesha madeni ya mikopo ya pembejeo kwenye Benki walizokopa kwa asilimia 100 jambo ambalo lilipelekea kushindwa kuwalipa wakulima wao kutokana na sabahu ya wakulima hao pia kutorosha tumbaku na kwenda kuiuza kwenye vyama vingine.
Kufuatia taarifa hiyo Mhe. Mndeme aliagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi wa tuhuma za viongozi na wakulima hao waliotenda hayo na kusababisha deni la zaidi ya Bilioni 2.5 na kwamba watoe taarifa ndani ya siku 30 kuanzia leo tarehe 17 Sept, 2023.
Aidha Mndeme alimuagiza Mrajis Msaidizi kuangalia na kupitia upya mikataba kati ya Vyama vya Msingi, Kampuni zinazonunua Tumbaku na Benki husika ili kuwaondolea mizigo ya madeni wakati inapotokea Kampuni inashindwa kulipa deni hilo jambo ambalo litakwenda kuwaondolea malimbikizo ya madeni wasiyostahili kuyalipa.
KACU LTD imesajiliwa tarehe 20 Aprili, 1994 chini ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na. 15 ya mwaka 1991 fungu la 30 kwa usajili namba 5493 ina wanachama 126 ambapo 36 ni wa zao la Pamba, 46 zao la Tumbaku na 44 wanashughulika na mazao yote mawili.
HABARI NA MATUKIO
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa