RC MNDEME ASHIRIKI SHEREHE NA MAADHIMISHO YA UPADIRISHO WA SHEMASI JAMES FURAHA MREMA.
Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Moa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme leo tarehe 6 Julai, 2023 ameshiriki katika maadhimisho ya upadirisho wa Shemasi James Mrema sherehe zilizofanyika katika Parokia ya Msalaba Mtakatifu - Mwadui hapa Mkoani Shinyanga.
Katika sherehe hizi ambazo zimeongozwa na Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo kuu Katoriki, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude na viongozi mbalimbali.
Mhe. Mndeme amesema kuwa Serikali inatambua, inathamini na kuheshimu michango yote inayotolewa na Taasisi za Dinini kiwamo Kanisa Katoriki hasa katika nyanja za Sekta ya Elimu, Afya, Ustawi wa Jamii nk huku akiahidi kuwapatia ushirikiano mkubwa Taasisi zote za Dini.
"Serikali yetu ya awamu ya sita inatambua, inathamini na kuheshimu michango yote itolewayo na Taasisi zote za Dini ikiwamo Kanisa Katoriki katika sekta ya elimu, afya, ustawi wa jamii nk," alisema Mhe. Mndeme.
Aidha Mhe. Mndeme amezitaka Jumuiya za Wanawake Wakatoriki Tanzania kuendelea kutoa malezi na kuimarisha makuzi ya watoto ili wasipotoke na kuiga tamaduni zisizofuata utu, utamaduni na mila za kitanzania.
Na kwamba Serikali ya awamu ya sita itaendelea kushirikiana na taasisi hizi katika kuwaletea maendeleo wananchi wake, ukizingatia kuwa Taasisi na Serikali zinamhudumia mtu huyo huyo mmoja isipokuwa majuku ndiyo yanatofautiana.
Kando na hayo Mhe. Mndeme pia alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wote wa dini kuendelea kumuombea heri, afya na maisha marefu Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani pamoja na wasaidizi wake katika kuwahudumia wananchi wa Tanzania huku akimuombea Padre James Mrema heri katika utumishi wake.
Wito umetolewa katika maadhimisho haya kuendelea kumuombea sana Padre James katika miito mitakatifu ili watenda kazi katika shamba la Bwana waongezeke zaidi, " Mavuno ni mengi, lakini watendakazi ni wachache. Basi mwombeni Bwana wa Mavuno, apeleke watendakazi katila mavuno yake". ( Mathayo 9:37 - 38)
Picha ikimuonesha MHE. Christina Mndeme akisalimiana na Baba Mshashamu Sangu baada ya sherehe za upadirisho
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa