• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
    • eVibali |
Shinyanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili Yetu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
      • Afya
    • Vitengo
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Shinyanga
    • Wilaya ya Kahama
    • Wilaya ya Kishapu
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
    • Halmashauri ya Mji wa Kahama
    • Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu
    • Halmashauri ya Wilaya ya Msalala
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Madini
    • Bandari Kavu
  • Huduma
    • Kutoa Ushauri wa Kitaalam
    • Kutafsiri Sheria na Sera
    • Kuratibu Shughuli za Wadau
    • Ulinzi na Usalama
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Fomu
    • Tafiti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha

RC MNDEME ATOA MWEZI MMOJA KWA MANISPAA YA SHINYANGA KUKAMILISHA UJENZI WA VYUMBA SOKO KUU

Posted on: September 11th, 2023

Na. Shinyanga RS

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme amesema hajaridhishwa na kasi ya ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga na kuagiza ifikapo tarehe 11 Oktoba, 2023 kuwa limekamilika kwa awamu ya kwanza ambayo ni milango iliyopo ghorofa ya chini.

Mhe. Mndeme ameyasema hayo leo alipofanya ziara ya kukagua ujenzi wa soko hilo, kuongea na wafanyabiashara, kusikiliza kero zao na kuzitatua ambapo pamoja na mambo mengine pia ameziagiza Halmashauri zote Mkoani Shinyanga kuhakikisha wanatenga chumba maalum ambacho kitatumika na wafanyabiashara wanawake wenye watoto ili waweze kuwanyonyesha watoto wao na kuwa sehemu sahihi kwa watoto hao kucheza wakati wazazi wao wakiwa katika biashara.

"Siwezi kusema nimeridhishwa, hapana niseme tu  kwamba sijaridhishwa kabisa na kasi ya ujenzi wa soko hili, niwaagize kufikia tarehe 11 Oktoba, 2023 ujenzi wa vyumba ghorofa ya chini uwe umekamilika ili wafanyabiashara waanze kazi zao haraka wapate kipato, na serikali ipate pato lake," alisema Mhe. Mndeme.

Ujenzi wa Soko Kuu la Manispaa ya Shinyanga wenye vyumba vya biashara 106 utagharimu Tzs. Bilioni 1.8 fedha kutoka mapato ya ndani ya Manispaa yatokanayo na makusanyo, ambapo mpaka sasa ni asilimia 56 ya ujenzi wote imekwishatekelezwa huku asilimia inayobakia inatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 11, 2023.

Baadhi ya picha zikionesha Mhe. Christina Mndeme akiwa katika soko kuu la manispaa ya shinyanga wakati wa alipotembelea kukagua, kuongea na wafanyabiashara, kusikiliza na kutatua kero zao. 



Matangazo

  • No records found
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • WANUFAIKA WA MIKOPO YA 10% LIPENI KWA WAKATI ILI PIA VIKOPESHWE NA VIKUNDI VINGINE - RC MACHA

    February 13, 2025
  • CP. HAMDUNI AKUTANA NA KAMATI YA MICHEZO YA JWTZ

    February 13, 2025
  • WANANCHI, LIPENI KODI YA ARDHI KWA WAKATI MUEPUKE RIBA - LEO KOMBA

    February 12, 2025
  • WAJUMBE WA BODI, TUMIENI TAALUMA ZENU KUISAIDIA HOSPITALI KUKAMILISHA MIRADI YA UJENZI- RAS CP. HAMDUNI.

    February 11, 2025
  • Angalia zote

Video

MIFUKO BANDIA ZAIDI YA ELFU 20 YAKAMATWA SHINYANGA
Video Nyinginezo

Viunganishi vya Haraka

  • Historia
  • Dira na Dhima
  • Hotuba Mbalimbali
  • Video Mbalimbali
  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Picha za Matukio
  • Miongozo na kanuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Ikulu
  • Mfumo wa kutuma, kupokea na kufuatilia malalamiko, mapendekezo, maulizo na pongezi
  • Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma
  • Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti Kuu ya Serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Boma Street, Mwanza Road

    Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga

    Simu: +255 28 2762222

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa