Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ameukaribisha kwa mikono miwili Uongozi wa Benki ya NMB Kanda ya Magharibi ambao walikuja Ofisini kwake kwa lengo la kujitambulisha huku akiwataka akiwashukuru sana kwa msaada wa Vifaa Tiba walivyotoa katika Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga.
Hayo yametokea leo tarehe 7 Agosti, 2023 ambapo Ndg. Seka Urio ambaye ni Meneja mpya wa NMB Kanda ya Magharibi alipofika Ofisini akiwa ameongoza na Ndg. Gadiel Sawe Meneja NMB Manonga Shinyanga, Bi. Vivian Nkhancaa ambaye ni Meneja Uhusiano Biashara na Huduma za Serikali Kanda ya Magharibi pamoja na Ndg. Emmanuel Makanga ambaye ni Meneja Uhusiano.
Mhe. Mndeme amewapongeza na kuwashukuru sana NMB Kanda ya Magharibi kwa msaada huo walio utoa kwa Serikali katika Sekta ya Afya na hasa kuichagua Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga jambo ambalo linakwenda kuborsha zaidi utoaji wa huduma bora kwa wananchi wa Shinyanga na maeneo jirani.
"Kwa dhati kabisa nawapongeza na kuwashukuru sana NMB Kanda ya Magharibi kwa msaada wenu wa kuboresha Sekta ya Afya katika Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga, mgeweza kuamua kuzitumia vinginevyo fedha hizo ukizingatia kuwa ninyi mnafanya biashara lakini mkaamua kuisapoti Serikali hakika umetenda jambo la kukumbukwa sana kwa wana Shinyanga na Serikali kwa ujumla wake tunawapongeza sana," alisema Mhe. Mndeme.
Kando na hayo, Mhe. Mndeme ametaka NMB kuangalia upya namna ya kuwawezesha vijana kwa masharti nafuu, hasa kwa kuwapatia vitendea kazi kama vile Mashine kubwa za kukoboa na kuchakata kwa lengo la kuongezea thamani mazao katika Mkoa wa Shinyanga.
Mhe. Mndeme pia amewataka NMB kujipanga kimkakati wakati ambapo Serikali inakwenda kutekeleza mredi wa kulifanya eneo lililokuwa na Buzwagi Wilayani Kahama kuwa Kanda ya Kiuchumi ili na wao NMB wawe tayari kuwekeza katika eneo hilo ambalo linatarajiwa kuwa kivutio kikubwa cha uwekezaji.
Kwa upande wake Meneja wa Kanda Ndg. Seka Urio alimshukuru sana Mhe. Mndeme kwa ukarimu wake, kwa kuwa tayari pia kuwapokea, alimpongeza sana kwa namna ambavyo anachapa kazi zake za kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Shinyanga huku akimuahidi kuwa maelekezo na ushauri wote alioutoa kwao wameuchukua na wataufanyia kazi kwa vitendo.
Mhe. Mndeme kwa niaba ya Serikali amekuwa na ushirikiano mzuri sana jambo ambalo linapelekea kuwa bega kwa bega kufanya kazi na Taasisi, Mashirika, Wadau na wananchi wote katika kuhakikisha kuwa wanawaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Shinyanga.
Picha ikionesha viongozi wa NMB Kanda ya Magharibi wakiwa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Mndeme
Baadhi ya vifaa tiba walivyokabidhi katika Hospitali ya Wilaya ya Shinyanga
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa