Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amejumuika na Waumini wa Kiislam Mkoani Shinyanga katika Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) iliyofanyika katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa ambapo alipata wasaa pia wa kueleza umma juu ya mafanikio yanayoletwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wa viongozi wa dini, Masheikh wakiongozwa na Sheikh Mkoa wa Shinyanga Sheikh Ismail Makusanya walimuombea Dua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwaongoza vema na kuwaletea maendeleo ya kweli watanzania wote kama yanavyojidhihirisha hapa Shinyanga kupitia Sekta mbalimbali.
Aidha pia, walimuombea pumziko la amani Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi, aliyekuwa Rais wa Awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyefariki tarehe 29 Februari, 2024 na kupumzishwa kwenye nyumba ya milele tarehe 2 Machi, 2024 visiwani Unguja.
Na tarehe 4 Machi, 2024 kutafanyika Ibada maalum ya kumiombea Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Sabasaba uliopo Manispaa ya Shinyanga.
HABARI PICHA
Picha ikimuonesha Sheikh Mkuu - Mkoa wa Shinyanga Ndg. Ismail Makusanya wakatiwa Maulid
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa