Na. Shinyanga RS
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ameongoza kongamano la Wanawake wa Mkoa wa Shinyanga la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mambo makubwa anayofanya kwa wanashinyanga katika kuwaletea maendeleo huku akiwataka kwenda na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi utakaofanyika mwaka 2025.
RC Mndeme amesema Mkoa wa Shinyanga wameua kumpongeza Rais wetu kwa sababu ya utekelezaji wake mzuri wa kazi kwa wqnanchi hasa katika kuwwletea maendeleo ambapo alisema vijiji vyote 506 vya mkoa wa shinyanga vimefikiwa kupitia sekta mbalimbali jambo ambalo limemsukuma yeye na kuumpa nguvu zaidi ya kuyasemea mazuri yote yqbayofabywa huku akisisitiza kuwa Shinyanga ya sasa siyo ya zamani.
"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo mengi yenye tija kwa watanzania na hasa wanashinyanga, hivyo leo tupo hapa kwa ajili ya kumpongeza na kuhakikisha tunakwenda nae mwaka 2025 na kuvuka nae kwakuwa shinyanga ya sasa siyo ya zamani na kila vijiji kimefikiwa na hakuna kilichosimama kazi inaendelea kwa vitendo,"alisema Mhe. Mndeme
Kwa upande wa viongozi kutoka mikoa jirani walisema kuwa, alichokifanya Mhe. Mndeme kimewaamsha sasa na wao kwenda kutekeleza katika mikoa yao huku wakimpongeza kwa ubunifu na uchapaji kazi wake katika kuwahudumia wananchi wa mkoa wa shinyanga ambapo maendeleo sasa yanaonekana kwa kasi.
RC Mndeme ameanzisha Kauli Mbiu isemayo "Kupitia utekelezaji mzuri wa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kila kijiiji kimefikiwa" akiwa na maana ya kuwa, hivi sasa mkoa wa shinyanya umefikiwa kila kijiji kupitia sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, maji, miundombinu, nishati, uwezeshaji wananchi kiuchumi, kilimo, mifugo
Katika kongamano hili ambalo liliongozwa, kusimamiwa na kutekelezwa na Mhe. Johari Samizi mkuu wa wilaya ya shinyanga, pia lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti CCM Mkoa wa Shinyanga ndg. Mabala Mlolwa, DC Mboni Mhita na wengine wengi kutoka mikoa jirani.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa