Na. Shinyanga RS.
MKUU wa mkoa wa shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule mpya ya Ngokolo Sekondari iliyopo kata ya Ndembezi, Skimu ya Umwagiliaji na jengo la utawala Manispaa ya Shinyanga huku akiwaagiza wahandisi wa Halmashauri zote za mkoa kuzingatia na kufuatilia ubora wa vifaa vyote vya ujenzi vinavyonunuliwa kwa ajili majengo ya serikali.
Agizo hili amelitoa mara baada ya kutilia shaka ubora wa bati zikizotumika kwenye ujenzi wa shule ya sekondari ngokolo ambapo bati lilionekana kuwa laini jambo ambalo lilileta shaka kwa Mhe Mndeme.
"Nawaagiza Wahandisi wa Halmashauri zote hapa Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha kuwa wanazingatia ubora na viwango vya vifaa vya ujenzi vinavyonunuliwa, na hii ni kwa mkoa mzima naagiza," alisema Mhe. Mndeme.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo alipokuwa akifanya majumuisho ya ziara yake iliyokuwa imejumuisha viongozi wa serikali na chama huku akiwasisitiza waandisi kutumia muda mwingi kukagua na kusimamia miradi yaserikali kwakuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa fedha nyingi kutekeleza miradi hii kwa maendeleo ya wananchi.
Huu ni muendelezo wa ziara zake za ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga, ambapo kwa Manispaa ya Shinyanga amekagua ujenzi wa shule ya ngokolo, mradi wa skimu ya umwagiliaji Kitangili na ujenzi wa jengo la Utawala ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na maelekezo yake kwa wataalamu, lakini ameridhishwa na utekelezaji wa miradi hii.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa