MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka wazazi na walezi wote mkoa wa shinyanga kuhakikisha wanawaleta watoto wao wote ambao wanastahili kusoma kwakuwa hakuna tena ada, kila mtoto anayestahili kusoma atapokelewa na hakuna hata mtoto mmoja atakayebakia nyumbani.
Mndeme ameyasema hayo leo tarehe 8 Januari, 2024 alipotembelea shule ya Awali na Msingi Mwenge, shule ya Sekondari Ngokolo pamoja na shule ya Sekondari Wasichana Shinyanga zote za Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine pia amewapongeza walimu wote wakiongozwa na Maafisa Elimu wao wote kwa kazi nzuri wanazozifanya ikiwàmo kufundisha, kuhamasisha na kuandisha watoto wapya.
"Nawaomba sana wazazi na walezi wote wenye watoto wanaostahili kusoma muwalete shuleni, hakuna atakayewadai ada, kuwarudishawala hamtapata usumbufu wowote, na hasa wenye ulemavu msiwafiche na kuwaacha nyumbani waleteni shuleni kila kitu ni bure", amesema Mhe. Mndeme.
Kando na wito huo, RC Mndeme amewaeleza wanahabari na walimu waliokuwa katika majumuisho ya ziara hii kuwa, Serikali ya mkoa wa shinyanga imefanikiwa kumuokoa mwanafunzi wa kidato cha kwanza 2024 (jina limehifadhiwa) aliyekuwa ameozeshwa na mzazi wake ajulikanaye kwa jina la Dotto Mjanasa maarufu kama Dullah Mjanasa mkazi wa kijiji cha Iyugi, Kata ya Lyamidati Halmashauri ya Shinyanga amabye alimuozesha kwa jumla ya ng'ombe 15.
Mtoto huyu ambaye amefaulu vizuri sana, amenusuriwa na serikali baada ya wasamalia wema kutoa taarifa a,bapo serikali ilichukua hatua ya harakaya kwenda eneo la tukio na baada ya kumkomboa mzazi huyoa alikimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea.
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Mwl. Dafroza Ndalichako amesema kuwa kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi ya 2022, mkoa ulikuwa na maoteo ya kuandikisha wanafunzi wa Awali 75,079 ambapo mpaka sasa wameandikisha wanafunzi 47,182 na kwa darasa la kwanza lengo ni 69,792 huku walioandikishwa ni 44,332 na kwa kidato cha kwanza ni 38,963.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa