Na. Shinyanga RS
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme leo tarehe 18 Septemba, 2023 ameweka Jiwe la Msingi katika Shule Mpya ya Sekondari Ngilimba iliyopo Kata ya Ulowa yenye thamani ya Tzs. Milioni 603 ambapo chanzo cha fedha ikiwa ni SEQUIP huku akiwataka wananchi kuitunza ili ije kuwanufaisha na vizazi vijavyo.
Akizungumza na wananchi wa Ngilimba Mhe. Mndeme alisema kuwa ameridhishwa sana na kasi ya ujenzi wa shule hii huku akisema kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeleta fedha nyingi sana katika Sekta mbalimbali ikiwemo Elimu ambapo Kijiji cha Ngilimba kinashuhudia ujenzi wa shule nzuri ya kisasa ambayo inakwenda kuwaondolea adha wanafunzi ya kutembea umbali wa zaidi ya Kilomita 10 hadi 17 walizokuwa wakitembea kuifuata sekondari ya Ulowa.
"Niseme tu kwa dhatiya moyo wangu kuwa, nimeridhishwa na kasi ya ujenzi wa Sekondari Mpya ya Ngilimba hapa Kata ya Ulowa ambapo zaidi ya Tzs. Milioni 603 fedha za SEQUIP, jambo kubwa niwaombe wananchi kuitunza shule hii ili iwanufaishe na vizazi vijavyo," alisema Mhe. Mndeme.
Katika ziara hii pia Mhe. Mndeme amefika Kijiji cha Bulega na kufanya mkutano mkubwa wa hadhara ambapo pamoja na mambo mengine amesikiliza kero na kuzipatia ufumbuzi ikiwemo kero ya kukosekana kwa usalama, kutolipwa fedha kwa wakulima wa tumbaku na kukosekana kwa mawasiliano yoyote.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani pamoja na pongezi nyingi kwa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea fedha nyingi katika miradi mbalimbali, lakini pia alimueleza Mhe. Mndeme juu ya uwepo wa changamoto ya maji japokuwa uwepo wa mpango wa kuletwa kwa maji ya Ziwa Victoria
Akitatua kero hizo Mhe. Mndeme ameagiza uongozi wa Wilaya ya Kahama kukamilisha haraka kwa Kituo cha Polisi Ulowa, kero ya mawasiliano amewaeleza wananchi hao kuwa hivi karibuni kutafungwa mnara wa Vodacom na tayari wamekwishafika Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Bulega hivyo wataanza kujenga mnara hivi karibuni.
PICHA NA MATUKIO
Mhe. Mndeme wa kwanza kushoto akifuatiwa na Mhe. Mboni Mhita DC Kahama pamoja na Mhe. Cherehani Mbunge wa Jimbo la Ushetu wakionesha kwa vitendo uwekaji vigae kama ishara ya hamasa kwa wananchi wa kijiji cha Ulega Kata ya Ulowa - Ushetu
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa