RC MNDEME AWEKA JIWELA MSINGI ZAHANATI YA SESEKO, WANANCHI WAMSHUKURU SANA MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Na. Shinyanga RS
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme ametembelea, kukagua na kuweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Kijiji cha Seseko iliyopo Kata ya Mwamalili Manispaa ya Shinyanga inayohudumia zaidi ya wakazi 2700 iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi mwaka 2007 ambapo baadae Serikali imekuja kutoa fedha za kukamilisha ujenzi huu wenye thamani ya zaidi ya Milioni 95 jambo ambalo linawafanya wananchi wa Seseko kumshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha hizi na kuwaondolea kero ya kukosa huduma kwa muda mrefu.
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la msingi Mhe. Mndeme amewaeleza wananchi hao kuwa, Serikali ya awamu ya sita imeleta fedha hizo katika Zahanati hii kwa lengo la kutatua kero hii ya muda mrefu iliyokuwa ikiwakabili wananchi hawa wakitokea Vitongoji vya Seseko, Nhohola na Ilugala ambapo huduma mbalimbali za afya kwa baba, mama na mtoto zinapatikana sambamba na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga katika cha Seseko na maeneo jirani kwa ujumla huku akiwataka kuitunza zahanati hii.
"Niwapongeze sana wana Seseko kwa kupata mradi huu wenye kija kubwa zaidi na hatima ya afya zetu, uwepo wa mradi huu unakuja kuondoa kabisa kero ya muda mrefu ya kufuata huduma hii mbali zaidi na sasa Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuja kuwaondolea kero hii, niwatake sasa niwatake kuitunza zahanati hii ili iwanufaishe na vizazi vijavyo ukizingatia nimekagua na kuona dawa zipo za kutoshq na huduma mnapata zote muhimu," alisema Mhe. Mndeme.
Awali wananchi wa Seseko wakiwa mbele ya Mhe mndeme walitoa Shukurani zao nyingi kwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasaidia kuondokana na kero hiyo ambayo imewasumbua kwa muda mrefu sana, na sasa wanasema hakuna tena kero hii jambo ambalo walimtaka Mhe. Mndeme kuhakikisha anazifikisha shukurani zao kwake Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungajpno wa Tanzania.
Zahanati ya Seseko imesajiliwa na Wizara ya Afyana imeshapata usajili wa MSD, imeanza rasmi kutoa huduma mwezi Agosti, 2023 ambapo huduma zinazoyolewa ni pamoja na huduma za wagonjwa wa nje (OPD), Kliniki ya Baba, Mama na Mtoto, huduma za chanjo pamoja na huduma za upimaji kwa baadhi ya magonjwa.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa