Na. Shinyanga RS.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Solomon Mndeme amizitaka Halmashauri zote ndani ya Mkoa wa Shinyanga kukamilisha ujenzi wa miradi ya Boost kabla ya tarehe 10 Julai, 2023 ili wananfunzi waweze kuanza kunufaika na miundombinu hiyo.
Mhe. Mndeme ameyasema hayo alikuwa akikagua ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu ya vyoo (3) katika Shule ya Msingi Busongo iliyoka Halmashauri ya Msalala na Shule mpya yenye jumla ya madarasa 16 inayojengwa Manispaa ya Kahama ambayo alipendekeza iitwe jina la SHULE YA MSINGI ANDERSON ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake mkubwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo Manispaa ya Kahama huku akiwaagiza viongozi wa Kamati za Shule na wananchi kuitunza miradi hiyo.
"Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametuletea fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ikiwamo hii ya Elimu, naziagiza Kamati za Shule zote Mkoani hapa kuhakikisha tumshukuru zaidi Mhe. Rais kwa kuilinda miundombinu hii ili ije kuwanufaisha na vizazi vijavyo na muhakikishe mnaikamilisha kabla ya tarehe 10 Julai, 2023 na hili ni kwa Halmashauri zote hapa Shinyanga," alisema Mhe. Mndeme.
Mkoa wa Shinyanga pamoja na mambo mengine, kwenye sekta ya elimu inajenga Shule za Msingi 9 mpya, madarasa 84 na matundu ya vyoo 133 ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Boost.
ReplyForward |
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa