Na. Shinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amuungana na viongozi wa dini mbalimbali wa Serikali pamoja na wananchi Mkoani Shinyanga katika dua na sala ya kumuombea pumziko la amani Hayati Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyefariki tarehe 29 Februari, 2024 huku akiwaomba wananchi wote kufika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kusaini Kitabu cha Maombolezo.
Dua na Sla hii imefanyika leo Machi 4, 2024 katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ambapo pamoja na kumuombea Hayati Ali Hassan Mwinyi, pia wameliombea Taifa linaloongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwahudumia vema na kuwaletea maendeleo yanayoonekana kama ilivyo kwa Mkoa wa Shinyanga.
“Ndugu zangu viongozi wa Dini, Serikali na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kutoka Madhehebu mbalimbali tumekusanuika hapa ili tumombee Dua na Sala Rais wetu Mstaafu Hayati Ali Hassan Mwinyi ili Mwenyezi Mungu ampokee katika Ufalme wake na ampatie pumziko la Amani,”amesema RC Mndeme.
RC MNDEME ameongeza kusema kuwa, tumuombee pia Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa msiba huu mzito ambao ameupata kwa kuondokewa na kiongozi mkubwa ambaye alikuwa akimtegemea pia katika ushauri mbalimbali namna ya kuongoza nchi na kuwatumikia watanzania huku akiwatakia faraja familia ya marehemu inapopitia kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga Ismail Makusanya, akizungumza kwenye maombi haya, amesema katika Mkoa huu hawatamsahau Hayati Mwinyi kwa kutatua mgogoro mkubwa ambao ulikuwapo wa kiimani, ambapo aliutatua na kudumisha amani.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa