Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewaka wananchi wa Wilaya ya Kahama kuendelea kushirikiana kujenga maboma ya shule ya Msingi Mayila iliyopo kata ya Nyihogo Wilayani Kahama kutokana na mahitaji makubwa ya madarasa.
Mhe. Telack ametoa wito huo jana tarehe 07 Januari, 2020 alipokuwa Wilayani Kahama kukagua utekelezaji wa agizo la Rais Mhe. John Pombe Magufuli la kuhakikisha shule hiyo aliyoichangia shilingi milioni 5 inafunguliwa.
Amemshukuru Mhe. Rais kwa kuhamasisha ujenzi wa shule hiyo kwa kuongeza nguvu na kufanya kuwe na mazingira mazuri kwa wanafunzi na walimu na kuwamasisha wananchi wawapeleke shule watoto wote wanaostahili kusoma.
“Wazazi leteni watoto wasome madarasa yanatosha, wakati wanasoma Serikali inaendelea kujenga madarasa mengine kwani ni jukumu la Serikali, lakini na wananchi nao waendelee kuongeza nguvu kujenga shule iwe kubwa” amesema Telack.
Telack pia amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Anderson Msumba na kamati yake ya ujenzi kwa kutekeleza agizo la Mhe. Rais kwa wakati.
“Tumekuja kuona kama shule hii imeanza kama alivyoahidiwa Mhe. Rais, tumekuta kweli shule imeanza, niwapongeze sana kwani msingetekeleza mngekuwa mmeniangusha mimi na Mhe. Rais” amesema Mhe. Telack.
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa