Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Zainab Telack amewataka wazazi kuwapeleka shule watoto wao ili waelimike na kusaidia kupunguza tatizo la mauaji ya vikongwe kwa imani za kishirikina.
Mhe. Telacka ametoa wito huo katika Kongamano maalumu lililoandaliwa na Kamati ya Amani ya Mkoa kwa ajili ya kuliombea Taifa na Mkoa katika uwanja wa Zimamoto, Manispaa ya Shinyanga.
Telack amesema kuwa, Serikali hivi sasa inapeleka fedha katika kila shule kwa ajili ya maendeleo badala ya kuwachangisha wazazi fedha, hivyo watumie fursa hiyo wawasomeshe watoto wao kwani kazi ya mzazi ni kununua sare na madaftari tu.
Amesema watoto wakielimika watatambua thamani ya vikongwe badala ya kuwauwa watawatunza.
Aidha, Mhe. Telack amesema malezi ndiyo msingi wa Amani katika nchi kwani amani na upendo huanzia kwenye familia hivyo wazazi na walezi washirikiane katika malezi ya watoto kwa kuzuia mimba za utotoni, mavazi yasiyofaa na matumizi yasiyo sahihi ya tekinolojia.
Amehimiza pia wananchi kulima kwa wingi ili kujiepusha na tatizo la njaa kwa sababu kukosa chakula pia ni chanzo cha kukosekana kwa amani katika jamii.
Shekh Soud akitoa maombi maalumu ya kuombea
Amani Mkoa wa Shinyanga na Nchi kwa ujumla katika kongamano hilo
Mchungaji Zakayo Bugota akiongoza maombi
ya kuombea Amani katika Kongamano hilo
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa