Na. Shinyanga RS.
KAMATI ya Ushauri ya Mkoa (RCC) Mkoa wa Shinyanga imepisha azimio la kumpongeza kwa dhati kabisa Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri na njema anayoifanya ya kuwaletea maendeleo wananchi wote wa Tanzania wakiwemo na wakazi wa Shinyanga.
Azimio hili limepisha katika kikao hicho tarehe 7 Machi, 2024 kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga na kuhudhuriwa na wanjumbe, viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi, viongozi wa Dini na wadau wa maendeleo ambapo pamoja na azimio hili lakini pia Mwenyekiti wa kikao hiki Mhe. Christina Mndeme amewataka Maafisa Mifugo kuwafikia wafugaji, kuwaelimisha na kuwasaidia namna bora ya kufuga kisasa, kutibu mifugo ili iwe yenye tija.
RC Mndeme pia ameziagiza Halmashauri zote kutenga eneo maalum kwa ajili ya kufugia na malisho lengo ni kuwawezesha wafugaji kuwa na mifugo mingi ambayo itakuwa inachinjwa na kusafiroshwa nje ya Mkoa wa Shinyanga ukizingatia Manispaa ya Shinyanga inayo machinjio ya kisasa kabisa lakini mifugo inaonesha kupungua.
RCC pamoja na mamno mengine, lakini pia imefikia uamuzi wa kukiomba Kiwanda kilichokuwa cha nyama ambacho kipo Manispaa ya Shinyanga na maeneo yake ili kirudishwe Manispaa na kuanza kuendeshwa na Halmashauri hii kwakuwa kilikuwa msaada mkubwa kwa wananchi.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobass Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira, na Wenye Ulemavu) ameshauri eneo lililopo Ndembezi kurejeshwa kwa wananchi ili wafanye maendeleo ukizingatia kuwa eneo hilo lwnye ukubwa wa zaidi ya hekari 5 hailitumiki kwa muda mrefu sasa.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa