Na. Sinyanga RS.
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina S. Mndeme leo tarehe 20 Novemba, 2023 akiwa ameongozana na wataalamu kutoka Tarura Mkoa na Wilaya ya Shinyanga ametembelea na kukagua miundombinu ya barabara na madaraja kwa ajili ya kuona uimara wake kabla ya mvua kubwa zinazotarajiwa kunyesha kwa mujibu wa Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Tanzania huku akimuagiza Mhandisi wa Tarura Wilaya ya Shinyanga kuhakikisha wanazibua na kusafisha mitaro pamoja na madaraja kabla ya mvuakuanza.
Mhe. Mndeme ametoa maagizo hayo mara baada ya kukagua madaraja mawili ya Kitangili, ujenzi wa barabara ya Kongo wa kiwango cha lami Mita 145 yenye thamani ya Milioni 88 iliyopo mtaa wa Lumumba, uzibuaji wa daraja la Tambukareli Kata ya Ndembezi hapa Manispaa ya Shinyanga na kuwataka wananchi kuhakikisha wanailinda nankuitunza miundombinu hii ili iwe msaada kwa sasa na baadae.
"Leo tumetembelea na kukagua miundombinu ya barabara na madaraja ambayo inqhudumiwa na Tarura, pamoja nq pongezi kwa kazi wanazozifanya, lakini niwatake Tarura kuhakikisha mnazibua na kusafisha mitaro yote pamoja na madaraja ili iwe tayari kukabiliana na mvua kubwa inayotarajiwa kunyesha kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania," alisema Mhe. Mndeme.
Kwa upande wake Mhandisi Samson Pamphili wa Tarura Wilaya ya Shinyanga alisema kuwa, wamepokea maagizo ya Mhe. Mndeme na kwamba watatekeleza haraka ili kwenda na wakati kwani tahadhari imekwishatolewa juu uwepo wa mvua kubwa.
Eng. Samson aliongeza kusema kuwa, wao Tarura wanaendelea na uzibuaji wa mitaro na usafishaji katika mji wote huku akiwataka wananchi kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kandokando ya miundombinu hii inayotekelezwa ili isiharibike na badala yake kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie ili iweze kudumu.
"Nitumie nafasi hii kuwaomba wananchi wote kuacha kufanya shughuli za kibinadamu kandokando ya miundombinu hii ili isiharibike, na badala yake tuitunze zaidi, na pia niwaombe viongozi wa serikali za mitaa wote wasaidie katika utoaji wa elimu hii kwa wananchi wao kupitia mikutano yao na vikao," alisema Eng. Samson.
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa