AFISA Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson amewataka watoto kuishi katika Maadili Mema na yenye hofu ya Mungu huku akiwapongeza pua kwa kushiriki kikamilifu katika maadhimisho ya siku ya mototo wa Afrika
Bi. Rehema amesena kuwa Serikali inatambua na kuthamini sana haki zenu lakini na wao watoto wanao wajibu wao kimsingi kama watoto kwa wazazi na Serikali na kwamba wakati inasemwa haki zao wakumbuke kabisa haki yako inaweza isiwe haki kama haujatimiza wajibu wao.
“Kauli mbiu ya Mwaka huu inasisitiza kuzingatia maarifa, maadili na stadi za kazi kwahiyo zingatieni stadi za kazi, maadili mema, kuweni raia wema, kuweni watoto wema kuweni waumini wema nyumbani, muishi kwa kutambua uwepo wa Mwenyezi Mungu, na mkipewa kazi na wazazi mzifanye achene kuzurula na Mungu atawasaidia sana kutimiza ndoto zenu," amesema Rehema.
Kwa upande wake Polisi Jamii kutoka Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Shinyanga Jane Mwazembe ametoa elimu kuhusu ukatili wa kijinsia na njia za kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili huku akisisitiza watoto kutoa taarifa wanapoona dalili za ukatili ambapo amewataka kutoa taarifa kwa mtu yoyote ambaye wanamwamini wakiwemo wazazi, walimu, maafisa ustawi wa jamii, pamoja na kutoa taarifa kwenye Serikali za Mitaa.
Aidha Mmwenyekiti wa Baraza la Watoto Mkoa wa Shinyanga ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Taifa Raphael Charles amewahimiza wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa watoto huku akisisitiza kuhakikisha watoto wanapata haki yao ya elimu ambayo ni muhimu katika maisha yao ya kila siku.
Mwenyekiti huyu ametumia nafasi hii pia kuipongeza Serikali kwa kuendelea kuthamini haki za watoto hali ambayo imesababisha kuimarishwa kwa huduma za kiafya kwa watoto, wakati huo huo ameiomba Serikali kuendelea kutatua changamoto zinazowakabili watoto nchini.
Kaulimbiu ya siku ya leo inahimiza utoaji wa elimu inayowajumuisha watoto wote, isiyobagua mtoto kutokana na hali yake (inclusiveness). Aidha, Elimu hiyo ilenge kumpatia mtoto Maarifa (elimu bora na ufaulu) Maadili (maadili mema, uadilifu na hofu ya Mungu) na Stadi za Kazi (kazi za mikono ipi kujenga ujuzi)
HABARI PICHA
Boma Street, Mwanza Road
Anuani: P.O.Box 320, Shinyanga
Simu: +255 28 2762222
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@shinyanga.go.tz
Hakimiliki@2018. Mkoa wa Shinyanga. Haki zote zimehifadhiwa